Kwa mujibu wa shirika la habari la Sama la Palestina, maafisa hao 12 waliojiuzulu wa serikali ya Marekani wameonya katika taarifa kwamba kushindwa siasa za Washington kuhusu Ukanda wa Gaza ni tishio kwa usalama wa taifa la Marekani.
Kwa mujibu wa maafisa hao, uungaji mkono wa Marekani kwa utawala katili wa Israel na kuutumia silaha kwa lengo la kuwaua Wapalestina ni kushiriki katika mauaji ya kizazi na kusababisha njaa kali kwa watu wa Ukanda wa Gaza.
Maafisa hao wamesema sera mbovu na zisizo za busara za nchi za Marekani na Magharibi kuhusu Gaza ni tishio kwa usalama wa Marekani na kwamba zinahatarisha maisha ya wanajeshi na wanadiplomasia wa nchi hiyo.Maafisa hao waliojiuzulu wa serikali ya Marekani, wanasisitizwa kuwa siasa za serikali ya Joe Biden kuhusu Gaza zimedhoofisha nafasi na itibari ya Marekani mbele ya walimwengu. Baada ya kupita takriban miezi 9 ya uvamizi usio na tija wa ukanda wa Gaza, utawala wa Kizayuni haujafanikiwa lolote zaidi ya kufanya mauaji ya umati, uharibifu, jinai za kivita, ukiukaji wa sheria za kimataifa, ulipuaji wa mashirika ya misaada ya kibinadamu na kusababisha njaa kwa watu madhulumu wa ukanda huo unaozingirwa kwa miaka mingi.
342/