16 Novemba 2024 - 16:27
Kituo cha kwanza cha elimu ya Kiislamu kwa lugha ya Kihispania kitafunguliwa huko «Alif», nchini Marekani

Kituo cha Elimu ya Kiislamu katika Wilaya ya «Alif», kilichopo Houston, Marekani, kitafungua rasmi milango yake kwa umma kwa ajili ya sherehe za ufunguzi.

Kulingana na Shirika la Habari la Ahlul-Bayt - ABNA - Kituo cha kwanza cha Sayansi (elimu) ya Kiislamu kinachotumia lugha ya Kihispania katika eneo la «Alif», kilichoko Houston, Marekani, kitafungua rasmi milango yake kwa umma kwa ajili ya sherehe za ufunguzi.

Kituo hiki kinahudumia haswa Waislamu wanaozungumza Kihispania na kinataka kuangazia uhusiano wa kihistoria kati ya Uislamu na Wahispania.

Kituo cha «Alif» cha Sayansi (Elimu) ya Kiislamu kilitangaza kwamba kitatoa rasilimali kadhaa kwa wale wanaopenda Uislamu na Waislamu wapya wanaozungumza Kihispania ili kugundua kilichowaongoza katika safari yao ya kiroho ya kutafuta (ukweli na uhakika).