16 Desemba 2024 - 14:30
Habari Pichani | Maandamano katika Mji wa "Katsina" nchini Nigeria kwa ajili ya kumbukumbu ya Mashahidi wa mauaji ya Zaria.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Maandamano yamefanyika katika mji wa "Gombe" nchini Nigeria kwa ajili ya kumbukumbu ya Mashahidi wa Mauaji dhidi ya Mashia katika Mji wa "Zaria" yaliyofanywa na jeshi la Nigeria mwaka 2015. Katika mauaji hayo ya Zaria, takriban watu elfu moja, ambao wengi wao walikuwa Wafuasi wa Shule (Madrasat) ya Ahl al-Bayt (a.s) waliuawa Kishahidi.

Watoto watatu wa Sheikh Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, pia walikuwa miongoni mwa Mashahidi wa mauaji hayo ya Zaria.