Akijibu ujumbe wa mtandao wa kijamii unaotetea hatua hiyo leo Jumapili, Musk, ambaye anaongoza Idara ya Ufanisi wa Serikali ya Marekani (DOGE), amesema, "Ninaafiki."
Rais wa Marekani, Donald Trump na wabunge wa chama cha Republican wameapa kutazama upya uanachama wa Washington katika Umoja wa Mataifa, na pia katika jumuiya ya kijeshi ya NATO, inayoongozwa na Marekani.
Mnamo Februari, Seneta Mike Lee wa Utah aliwasilisha mswada wa Sheria ya Kujitenga Kabisa na Mtanziko wa Umoja wa Mataifa ya (DEFUND), akipendekeza kujiondoa kikamilifu kwa Marekani kutoka Umoja wa Mataifa.
Lee aliukosoa Umoja wa Mataifa na kulitaja kama "jukwaa la madhalimu" ambalo linaihujumu Marekani na washirika wake, akisema kuwa licha ya ufadhili mkubwa kutoka Washington, lakini shirika hilo limeshindwa kuzuia vita, mauaji ya halaiki, ukiukaji wa haki za binadamu na majanga.
Akirejelea matamshi hayo ya Seneta Lee, Musk ameandika kwenye mtandao wa X kwamba, "Marekani hutoa ufadhili mkubwa kwa UN na taasisi zinazofungamana nayo."
Msimamo wa bilionea huyo unalandana na wa Trump, ambaye mara kwa mara amekuwa akiikosoa NATO, akiwataka wanachama wa jumuiya hiyo kuongeza bajeti za ulinzi, na kutishia kujiondoa, akisema Marekani inabeba mzigo usio wa haki wa kifedha kwa usalama wa Ulaya.
342/
Your Comment