Majid Takht Ravanchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Kigeni kisiasa ameandika katika mtandao wa kijamii wa X, akiashiria mkutano wa "Historia ya Uhusiano wa Kitamaduni na Kidiplomasia kati ya Iran na Austria" uliofanyika Jumanne katika Chuo Kikuu cha Tehran, kwamba moja ya vipengele muhimu vya uhusiano wa Iran na Austria ni ushirikiano wao wa kitamaduni, ambao unaweza kuwa kama daraja la kuunganisha mataifa haya mawili.
Ravanchi ameongeza kuwa: Kuwepo Wairani waliosoma nchini Austria kunaweza kuwa sababu ya kuimarishwa zaidi uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizi mbili.
Katika kipindi cha miongo minne iliyopita, Marekani imekuwa ikitekeleza kwa njia mbalimbali sera na hatua nyingi za upande mmoja dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kama vile kuweka vikwazo vya kiwango cha juu zaidi, vitisho vya kijeshi, kuanzisha kampeni za kisiasa na kidiplomasia na vita vya kisaikolojia dhidi ya Iran.
Licha ya kutokuwa na tija kwa sera na hatua hizo za upande mmoja za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, lakini bado Washington inasisitiza juu ya kuendeleza mbinu hiyo haramu na iliyo kinyume cha sheria pamoja na Hati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Tehran.
342/
Your Comment