Abdel Bari Atwan ameelezea kushangazwa na tabia ya baadhi ya nchi za Kiarabu ambazo zinajaribu kuisifu Marekani wakati ambapo uhakika ni kwamba Trump na serikali yake wamelazimika kupigia magoti msimamo wa kutotereka wa Muqawama wa Palestina. Amesema: Uamuzi wa Marekani wa kukubali kufanya mazungumzo na HAMAS, ni matokeo ya kukata tamaa na kuelewa kwamba hawawezi kuwalazimisha Wapalestina wanamuqawama kutii amri zao.
Ameongeza kuwa: Hatua ya Trump ya kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Hamas imekuja baada ya kutambua kwamba harakati hiyo haiogopi vitisho vyake na wala haiogopi kufunguliwa milango ya Jahannamu dhidi yake. Msimamo wa HAMAS ni imara na madhubuti. Wananchi wa Palestina nao wako imara na ndio maana njama za Trump zikiwemo za kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina kwenye Ukanda wa Ghaza, zimefeli.
Kwa mujibu wa mchambuzi huyo maarufu wa ulimwengu wa Kiarabu, vitisho vya kuendelea utawala wa Kizayuni wa Israel kuwaua kwa umati Wapalestina kwa kutumia mabomu ya Marekani navyo vimeshindwa. Amesema: Tofauti na wanavyojaribu kuonesha baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu, mazungumzo baina ya Marekani na HAMAS si zawadi, bali yamekuja baada ya Marekani kukata tamaa na kushindwa mbele ya msimamo usiotetereka wa Muqawama wa Palestina.
342/
Your Comment