Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Maulana Sheikh Hemed Jalala, Kiongozi Mkuu wa Shia Ithna Ashari Tanzania (T.I.C) ,akiongozana na watumishi wa Hawza ya Imam Sadiq (a.s) iliyopo Kigogo Post, Dar-es-Salam Tanzania, amefanya ziara muhimu katika Kituo cha kulea Watoto Yatima kilichopo Wipahs - Kibaha, na vile vile Kituo cha Afya cha Midwell, pamoja na Mradi wa Nyumba Maalum za Makazi zinazojengwa chini ya Usimamizi wa Mzee Haji Sahib.
Maulana Sheikh Jalala, alimpongeza Mzee Haji Sahib kwa kuendelea kuwajali na kuwatunza Mayatima, na kwamba utaratibu huu ni mwitikio mzuri wa maelekezo ya Dini Tukufu ya Kiislamu, ambayo daima inawataka Waislamu kuwapenda na kuwajali Mayatima.
Akisisitiza juu ya umuhimu wa kuwapenda na kuwajali mayatima amesema: Nijukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha anamkumbusha mwenzake juu ya kuwapenda na kuwajali Mayatima na kutatua changamoto zao mbalimbali na kuwatimizia mahitaji yao. Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) na Maimam wetu Watukufu wa Kizazi Kitukufu cha Mtume wetu Muhammad (amani iwe juu yao) walikuwa wakiwapenda na kuwajali Mayatima, na wametufundisha kwa vitendi namna ya kuwapenda na kuwathamini Mayatima.
Kila Muislamu, Uislamu unamuhimiza kulingatia suala hil, kwa sababu ikiwa leo hii hutomjali mtoto wa mwenzio, unamuona na kumpuuza na kumpita kwa sababu ni Yatima, vipi watoto wako ikiwa nao kesho watakuwa Mayatima?!.







Your Comment