Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran, Esmaeil Baghaei aliyasema hayo jana Ijumaa, siku moja baada ya Wizara ya Fedha ya Marekani kutangaza vikwazo dhidi ya Paknejad na mashirika matatu yanayojishughulisha na biashara ya mafuta ya Iran nchini China.
Vikwazo hivyo vipya vinakuja baada ya kukabidhiwa kwa barua ya Rais wa Marekani Donald Trump kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
Katika mahojiano na Fox News wiki iliyopita, Trump alitishia hatua za kijeshi dhidi ya Tehran ikiwa haitashiriki katika mazungumzo juu ya makubaliano mapya ya nyuklia.
Baghaei amesema vikwazo hivyo vipya vinaenda kinyume na madai ya mara kwa mara ya maafisa wa Marekani kuhusu utayarifu wao wa mazungumzo, na yanaonyesha uadui wa Marekani kwa maendeleo, na ustawi wa watu wa Iran.
Aidha amebainisha kuwa, "uraibu" wa Marekani kwa sera ya vikwazo na mashinikizo dhidi ya nchi huru unakiuka utawala wa sheria katika ngazi ya kimataifa na ni tishio kwa amani na usalama wa kimataifa.
Jana Ijumaa pia, wanadiplomasia wa China na Russia walitoa wito wa kuondolewa "vikwazo visivyo halali" dhidi ya Iran, wakisisitiza kuwa Tehran ina haki ya kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani. China, Russia na Iran zimesisitiza udharura wa kufanyika mazungumzo kwa msingi wa kuheshimiana pande mbili.
342/
Your Comment