Televisheni ya al Aqsa ni chaneli ya lugha ya Kiarabu ya Palestina yenye mfungamano na harakati ya Hamas yenye makao yake Ukanda wa Gaza kwenye satelaiti zote za mawasiliano.
Hamas imetoa taarifa na kuitaja hatua ya pamoja ya Marekani na Umoja wa Ulaya kuwa ni jaribio la kuzima sauti za Wapalestina na kuwazuia kuwasiliana na ulimwengu wa nje.
Taarifa ya Hamas imeongeza kuwa: Hatua ya Marekani na Umoja wa Ulaya ya kupiga marufuku matangazo ya Televisheni ya al Aqsa ni ukiukaji wa wazi wa uhuru wa vyombo vya habari na haki halali ya Wapalestina ya sauti yao kusikika duniani kote.
Taarifa ya Hamas imesisitiza kuwa: Hatua ya Marekani dhidi ya Televisheni ya al Aqsa ni uamuzi ulio kinyume na sheria dhidi ya vyombo huru vya vya habari vya Palestina vinavyofichua kwa jamii ya kimataifa mateso ya Wapalestina na jinai za Wazayuni.
Hamas imesema sauti ya Wapalestina itaendelea kuwa hai na itaendelea kuhami haki halali za Wapalestina hadi kupatikana haki zao zilizoghusubiwa, na wananchi hao kuwa huru kutoka katika makucha ya undamizaji wa Wazayuni.
Wakati huo huo, harakati ya Jihad Islami ya Palestina imelaani marufuku dhidi ya Televisheni ya al Aqsa na kukitaja kitendo hicho kuwa ni mzingiro mpya wenye lengo la kukandamiza sauti ya Wapalestina na kuwazuia raia hao kufikisha ujumbe wao kwa ulimwengu kuhusu mateso na masaibu wanayopitia kutokana na mashambulizi na ukandamizaji wa Israel.
342/
Your Comment