16 Machi 2025 - 17:50
Source: Parstoday
Iran: Marekani haina haki ya kutupangia tufuate siasa gani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe akisisitiza kuwa, Marekani haina haki ya kutupangia tufuate siasa gani za kigeni.

Sayyid Abbas Araghchi ameandika hayo leo Jumapili kwenye mtandao wa kijamii wa X na kuongeza kuwa, Marekani haina haki yoyote ya kuipangia Iran ifuate siasa gani za kigeni. Hayo yalimalizika tangu mwaka 1979 (baada ya kupatikana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kuundwa Jamhuri ya Kiislamu).

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia amesema: Mwaka jana Biden (rais aliyepita wa Marekani) aliupa dola bilioni 23 utawala katili wa Kizayuni unaoua kwa umati watu wasio na hatia na unaoangamiza kizazi. Matokea ya msaada huo wa Marekani ni kwamba Wapalestina zaidi ya 60,000 wameuawa na hivi sasa dunia inailaumu Marekani kuwa ndiye muhusika wa jinai hiyo ya kutisha.

Katika ujumbe wake huo wa leo kwenye mtandao wa kijamii wa X, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amewakhutubu viongozi wa Marekani akiwaambia: Komesheni kuunga mkono mauaji ya kizazi na ugaidi wa Israel. Acheni kuua raia wa Yemen.

Awali, Sayyid Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikukwa ameandika katika ujumbe wake akijibu matamshi ya vitisho ya Trump kuhusu kuilazimisha Iran kufanya mazungumzo kwamba: "Mazungumzo ni tofauti na utumiaji wa mabavu na kushurutisha. Hatutafanya mazungumzo chini ya mashinikizo na vitisho. Mazungumzo kama hayo hayafai hata kujadiliwa, haijalishi ni mada gani (ya kujadiliwa)."

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha