16 Machi 2025 - 17:52
Source: Parstoday
Wanawake wa Iran wanastawi kwa kasi licha ya vikwazo

Licha ya vikwazo, wanawake wa Iran wanaendelea kuwa na azma thabiti ya kujenga mustakabali wa haki zaidi.

Hayo yamesemwa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa Bi. Zahra Ershadi ambaye amefafanua kuhusu ustahimilivu na azma thabiti na isiyotetereka ya wanawake wa Iran katika kutengeneza mustakabali bora, wakati wa kikao cha 69 cha Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake kilichofanyika New York.

Katika hotuba yake, Ershadi amesisitiza dhamira ya Jamhuri ya Kiislamu ya kuboresha haki za wanawake na mchango wao mkubwa katika kuimarisha jamii na familia za Iran.

Ershadi amesema kuwa, licha ya athari mbaya za sera ya vikwazo na mashinikizo ya juu kabisa ambaye imefeli, wanawake wa Iran wanaendelea kupiga hatua za maendeleo na kuimarisha familia na jamii zao.

Akitilia mkazo jukumu muhimu la wanawake katika maendeleo ya kijamii, kitamaduni, kisiasa, na kiuchumi, Ershadi ametaja hatua kubwa zilizopigwa katika kulinda haki za wanawake katika sekta mbalimbali nchini Iran.

Wanawake sasa ni asilimia 33 ya wafanyakazi wa vyuo vikuu, asilimia 40 katika sayansi ya matibabu na zaidi ya asilimia 50 katika sekta jumla ya afya. Aidha, asilimia 40 ni madaktari bingwa na asilimia 30 ni madaktari bingwa wa juu zaidi. Wanawake pia wanaunda asilimia 45 ya wafanyakazi wa sekta ya umma, asilimia 74 ya sekta binafsi, na wanamiliki biashara 32,000. Kila mwaka, wanawake 300,000 wa vijijini na wale wa jamii za kuhamahama hupokea mafunzo ya ujasiriamali, na asilimia 41 ya nafasi mpya za kazi zimechukuliwa na wanawake.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha