19 Machi 2025 - 18:29
Source: Parstoday
Hamas: Marekani ni mshirika wa moja kwa moja katika vita dhidi ya watu wa Gaza

Msemaji wa harakati ya Hamas amesema harakati hiyo inatekeleza kikamilifu masharti ya makubaliano ya usitishaji vita na kwamba Wazayuni wameyakiuka akisisitiza kuwa, uratibu wa awali wa utawala huo ghasibu na Washington wa kuanzisha tena vita dhidi ya watu wa Gaza unaashiria ushiriki wa moja kwa moja wa Marekani katika jinai zinazofanywa Wazayuni.

Ni baada ya utawala katili wa Israel kuanzisha tena mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza huko Palestina na kuua mamia ya watu wasio na hatia. 

Akizungumzia kuanzishwa tena mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza, Abdul Latif Al-Qanou', msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), ametangaza kwamba kwa uratibu wa awali na Marekani, utawala ghasibu wa Israel umeanzisha tena vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza na kufanya jinai nyingi.

Msemaji wa Hamas ameongeza kuwa: "Uratibu wa hapo awali kati ya utawala wa Kizayuni na Marekani unaashiria ushiriki wa moja kwa moja wa Washinton katika vita hivyo na uungaji mkono wake kwa jinai zinazofanywa na Wazayuni. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kinyume na makubaliano ya kusitisha mapigano, ameanzisha tena vita dhidi ya Gaza ili kuepuka mgogoro wake wa ndani na kuweka masharti mapya katika mazungumzo hayo."

Al-Qanou' amesisitiza kuwa: Hamas imefuata masharti yote ya makubaliano ya usitishaji vita lakini adui Mzayuni amekataa kuyatekeleza.

Afisa huyo wa Hamas amesisitiza zaidi kuwa, jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua za haraka ili kusimamisha umwagaji damu katika Ukanda wa Gaza na kuwawekea mashinikizo Wazayuni.

Baada ya vita vya Gaza kusimama kwa muda wa miezi miwili kufuatia makubaliano ya usitishaji mapigano, mapema Jumanne, utawala wa Israel ulitangaza kuwa umeanzisha tena vita dhidi ya Gaza.

Takwimu za hivi karibuni kutoka Wizara ya Afya ya Gaza zinasema, watu 356 wameuawa shahidi katika mashambulizi hayo ya kikatili, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto na mamia zaidi wamejeruhiwa.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha