Taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imetolewa kutokana na kushadidi mashambulizi ya kijeshi ya Israel dhidi ya Syria na Ghaza. Wizara hiyo ya Saudia imessema, Riyadh inalaani vikali njama za Israel za kuyumbisha usalama na utulivu nchini Syria na katika eneo hili zima kwa kukiuka mara kwa mara mikataba na sheria za kimataifa.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia imesisitiza kuwa: "Jamii ya kimataifa lazima isimame imara kukabiliana na hujuma hizo za Israel, na kwamba nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa nazo zinapaswa kutekeleza jukumu lao na kusimama kidete kukabiliana na hujuma hizo za Israel illi kuzuia kuenea migogoro."
Vilevile taarifa ya wizara hiyo ya mambo ya nje ya Saudi Arabia imesisitizia haja ya kuamsha mifumo ya mashtaka ya kimataifa dhidi ya Israel katika kukabiliana na jinai zake hizo.
Taarifa hii imetolewa baada ya vyombo vya habari vya Syria kuripoti kwamba ndege za kivita za Israel zimeshambulia viunga vya mji wa Homs huko Syria, mashambulizi ambayo yamesababisha miripuko kadhaa kwenye viunga hivyo.
Baadhi ya duru za habari za Syria zimeripoti kuwa katika uvamizi wake mpya dhidi ya Syria Isrel imeshambulia kambi za kijeshi katika maeneo ya Shinshar na Shamsin ya kusini magharibi mwa Homs.
342/
Your Comment