Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni, Netanyahu amesema kuwa majeshi ya Israel yatashambulia Gaza kwa "kuongeza nguvu" na kwamba mashambulizi ya hivi karibuni ni hatua ya awali tu ya hujuma kubwa dhidi ya Harakati ya Muqawama ya Palestina Hamas na wakazi wa Gaza.
"Hamas tayari wamehisi uzito wa kikosi chetu katika saa 24 zilizopita, na ninataka kuwahakikishia - na wao - huu ni mwanzo tu," Netanyahu amesema, akisisitiza kwamba mazungumzo ya baadaye ya kusitisha mapigano yatafanyika "tu chini ya moto."
Matamshi ya Netanyahu yanakuja kufuatia wimbi jipya la mashambulizi ya anga ambayo yamesambaratisha usitishaji mapigano ambao tayari ulikuwa ni dhaifu, na ambao ulikuwepo tangu Januari 19.
Ametaja malengo ya utawala huo katika mashambulizi ya hivi sasa, ambayo ni pamoja na kuachiliwa kwa mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas, kusambaratisha kikamilifu kundi la Muqawama, na kuondoa vitisho vyovyote vinavyodaiwa kutoka Gaza hadi Israel. Malengo haya yamekaririwa katika kipindi cha miezi 17 iliyopita, lakini matokeo pekee yamekuwa uharibifu wa Gaza na kuhamishwa kwa wakazi wake.
Jamii ya kimataifa imeghadhabishwa na hatua ya utawala katili wa Israel kuendeleza mashambulizi ya anga dhidi ya Gaza, huku ikivunja makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyokuwa na lengo la kumaliza mzozo wake wa miezi 17 na Hamas.
342/
Your Comment