Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (A.S.) - Abna -; Mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya nchi hii yameingia wiki ya pili. Kuhusiana na hili, mji wa Hodeidah, ulioko Magharibi mwa Yemen, ulilengwa na mashambulizi kadhaa ya anga. Mashambulizi haya yalijumuisha mashambulio matatu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hodeidah, Kusini mwa mji huo, pamoja na kulenga eneo la Al-Manzar.
Abdul Malik al-Houthi, Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah, katika kujibu tangazo la Marekani la kupeleka shehena nyingine ya ndege kwenye Bahari Nyekundu, alichukulia hatua hii kuwa ni ishara ya kushindwa kwa chombo cha awali cha Marekani cha kubeba ndege cha Truman. Alisema kuwa Marekani inajaribu kuwatisha wengine kwa meli zake za kubeba ndege za kivita, lakini mbele ya Yemen, shehena hizo za kubebea ndege za kivita zinaweza kuwa mzigo mzito kwao (kwa Marekani).
Al-Houthi ameongeza kuwa Marekani iliweza kutishia nchi kubwa kupitia meli zake za kubeba ndege za kivita hapo awali, lakini imejiweka katika hali dhaifu mbele ya Yemen.
Wakati huo huo, vyanzo vya ndani vya Yemen vimeripoti kuwa Ansarullah ilirusha kombora la Balistiki kutoka Mkoa wa Saada kuelekea katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (na utawala haram wa Israel) siku ya Jumamosi jioni. Vyombo vya habari vya Kiebrania pia vilitangaza kwamba kombora hilo lilirushwa kutoka Yemen kuelekea Israel, na Idhaa ya Kiebrania 14 iliripoti kwamba kombora hili lilionekana kurushwa kuelekea kwenye meli katika Bahari Nyekundu.
Mapema siku ya Jumamosi, Harakati ya Ansarullah ilitangaza kuwa ililenga uwanja wa ndege wa Ben-Gurion kwa Kombora la "Palestine 2" la masafa marefu. Yahya Saree, Msemaji wa Kijeshi wa Ansarullah, alitangaza katika taarifa yake kwamba wanajeshi wa Yemen walilenga uwanja wa ndege wa Ben-Gurion katika eneo la Jaffa kwa Kombora la Balistiki la "Palestine 2" aina ya Hypersonic (ni kombora la Balistiki lenye mwendokasi zaidi ya kasi ya sauti).
Pia alionya mashirika yote ya ndege kuwa Uwanja wa ndege wa Ben Gurion hauko salama tena kwa safari za ndege na hali hii itaendelea. Ameongeza kuwa jeshi la ndege za anga zisizo na rubani la Yemen pia limefanya operesheni dhidi ya idadi ya meli za kivita zilizounganishwa na meli ya kubeba ndege ya USS Harry Truman.
Tangu jioni ya Jumamosi iliyopita, jeshi la Marekani limekuwa likifanya mashambulizi ya anga katika miji na maeneo mbalimbali ya Yemen, na mashambulizi hayo yamepelekea makumi ya watu kuuawa shahidi wakiwemo wanawake na watoto na kuharibiwa majengo na kukatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo. Wakati huo huo, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kwamba Iran inapaswa kuwajibika kwa kila risasi inayorushwa na Wahouthi wa nchini Yemen.
Tangu Novemba 2023, wanajeshi wa Yemen wameendeleza mashambulizi yao kwa kutumia makombora ya balistiki, ndege zisizo na rubani, na boti za baharini dhidi ya meli za Israel, Marekani, na Uingereza katika Bahari Nyekundu, Ghuba ya Aden na Bahari ya Arabia, na vikosi hivi vimelenga mara kwa mara maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na utawala haram wa Kizayuni. Vitendo hivi vinafanyika katika mfumo wa kile wanachokiita "Vita vya Ushindi Ulioahidiwa na Jihadi Tukufu".
Kuhusiana na hilo, siku ya Jumamosi, wanajeshi wa Yemen waliwazika wapiganaji wao wanane waliouawa shahidi katika siku za hivi karibuni. Kulingana na shirika la habari la Saba, marasimu hii ya mazishi ilifanyika kwa uwepo wa maafisa kadhaa wa kijeshi. Vyombo vya habari vya vita vya Yemen havikutoa habari yoyote kuhusu wakati na mahali pa kuuawa shahidi kwa watu hawa na vilionyesha tu kwamba walikufa katika "njia ya kutetea uhuru wa kitaifa".
Idadi ya Mashahidi wa Jeshi la Yemen katika mashambulizi ya anga ya Marekani na mapigano na vikosi vingine imefikia watu 52 tangu mwanzoni mwa Mwezi huu.
Your Comment