Mazoezi hayo yaliyoanza leo Alkhamisi katika maji ya Ghuba ya Uajemi, eneo la pwani la Makran na Bahari ya Caspian, yanafanyika sambamba na maandalizi ya Iran ya Siku ya Kimataifa ya Quds itakayoadhimishwa kote duniani Ijumaa ya kesho.
Luteka hiyo inajumuisha manowari na meli mbalimbali za Iran, ikiwa ni pamoja na meli ya kubeba ndege zisizo na rubani ya Shahid Baqeri, manowari ya Shahid Rais Ali Delvari, na boti za mwendo kasi za Jeshi la Wanamaji la IRGC, pamoja na vitengo vya kiraia vya baharini.
Admeli Alireza Tangsiri, Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC amesema kwamba takriban meli 3,000 nzito na nyepesi, zinashiriki katika maneva hayo ya kijeshi.
Ameeleza bayana kuwa, "Hatutaelekeza tu vita vyetu katika nchi kavu, enyi Wazayuni mnaoua watoto; tuko tayari baharini, na hamtakuwa na njia ya kutoroka."
Amesema mazoezi hayo ya kijeshi yanalenga hasa kuonyesha uwezo wa baharini wa mrengo wa Muqawama na kufikisha ujumbe kwa utawala katili na dhalimu wa Israel.
Tangsiri amesema jeshi la wanamaji la IRGC linafuata miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei na "litageuza bahari kuwa jahanamu kwa Wazayuni na kuifuta Israel katika uso wa dunia."
342/
Your Comment