27 Machi 2025 - 15:45
Source: Parstoday
Ndege za kivita za Trump haziwezi kuipigisha magoti Yemen

Chombo kimoja cha habari cha Marekani kimeandika makala ya uchambuzi na kusema kuwa, mashambulizi ya kijeshi ya Marekani, Israel na washirika wao kamwe hayawezi kulipigisha magoti taifa la Kiislamu la Yemen.

Shirika la Habari la Fars limenukuu makala hiyo kutoka kwenye jarida la Foreign Policy la Marekani inayosema: ndege za kivita za Trump haziwezi kukabiliana na wananchi mashujaa wa Yemen na kuongeza kuwa, Yemen si nchi ambayo Marekani inaweza kuishinikiza au kuilazimisha kukubali matakwa yake kupitia mashambulizi ya kijeshi.

Jarida hilo la Marekani limekiri pia kwamba kundi ya Muqawama la Ansarullah linafanya mambo yake kwa kujitegemea ingawa lina msimamo mmoja na Iran wa kuliunga mkono taifa la palestina Palestina na kupambana na Marekani na utawala wa wa Kizayuni wa Israel. Gazeti hilo limeandika: Tishio la Mahouthi dhidi ya utawala wa Kizayuni limepata nguvu tena kutokana na kuporomoka usitishaji vita huko Ghaza.

Uchambuzi wa jarida hilo la Marekani umezungumzia pia uwezo wa kidiplomasia na wa mazungumzo wa harakati ya Ansarullah na kufanikiwa kwake kuunda mtandao wa uhusiano mkubwa na nchi zingine hasa Russia na China na kusisitiza kwamba, hakuna uwezekano kabisa wa kuweza Marekani na washirika wake kuwashinda Wayemen kupitia mashambulio ya kijeshi.

Inafaa kukumbusha hapa kwamba mwaka 2019, Ansarullah ilishambulia na kusambaratisha miundombinu ya mafuta ya Saudi Arabia na kufanikiwa kuzima nusu ya uzalishaji wa mafuta kwa muda wa wiki mbili hadi tatu. Pia iliushambulia Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kutumia droni na makombora yaliyopiga shabaha kwa usahihi na ustadi mkubwa. Mafanikio hayo ni muhimu sana kwa nchi ambayo imewekewa vikwazo vya kila upande na haipati misaada ya kimataifa ya kijeshi.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha