Akijibu swali la ripota wa IRNA leo Alkhamisi, Baghaei amesema kuwa, kauli ya Kallas "haina msingi wala mantiki, ya kinafiki, na si ya kuaminika. Amesema Umoja wa Ulaya unapaswa kushughulikia mauaji ya halaiki na uchokozi wa utawala wa Israel dhidi ya nchi za eneo hili badala ya kutoa madai ya "kinafiki" dhidi ya Tehran.
Kallas alidai karibuni kuwa Iran ni "tishio" kwa utulivu wa kieneo na kimataifa na kwamba Tehran haipaswi kamwe kuruhusiwa kupata silaha za nyuklia. Alitoa madai hayo yasiyo na msingi katika mkutano na waandishi wa habari mjini al-Quds akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Gideon Sa'ar, ambapo pia aliituhumu Iran kwa kuunga mkono Russia katika vita na Ukraine.
Baghaei amesema iwapo Mkuu wa Sera za Kigeni wa EU anajali sana utulivu na usalama wa kikanda, angelishughulikia masuala kama vile mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza, uvamizi wa (utawala huo haramu) wa mara kwa mara dhidi ya Lebanon na Syria, na ukaliaji wa mabavu wa maeneo ya Asia Magharibi.
"Bi. Kallas, tofauti na watangulizi wake ambao walijaribu kutoa mtazamo wa muda mfupi katika kanuni za sheria za kimataifa wakati wa kutangaza misimamo ya Umoja wa Ulaya, anazungumza kwa ujasiri kwa namna ambayo, hata ikiwa inatokana na kutokuwa na uzoefu, anazidi kuharibu sura na uaminifu wa Ulaya mbele ya waangalizi wasio na upendeleo," amesema.
Baghaei amelaani sera za undumakuwili za Umoja wa Ulaya na kusisitiza kuwa, matamshi ya Kallas hayana msingi wala mantiki na madai yake ya kinafiki dhidi ya Iran hayana itibari.
342/
Your Comment