Kwa mujibu wa IRIB, Ramadan Sharif amesema hayo mbele ya waandishi wa habari jana Jumatano, Aprili 26, 2025 na kusisitiza kuwa suala la kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Palestina ni la wajibu na kwamba Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu itabebwa na kaulimbiu ya "Tuko kwenye Ahadi Ewe Quds." Amesema: Katika maadhimisho ya siku hiyo (ambayo ni Ijumaa ya mwisho ya Ramadhani na ambayo mwaka huu itakuwa ni Ijumaa ya wiki hii), tutawakumbuka kwa kheri mashahidi wa njia ya Quds; tutawakumbuka mashahidi wa Sayyid Hassan Nasrullah, shahidi Haniyeh, shahidi Yahya Sinwar na makumi ya mashahidi wa Kambi ya Muqawama.
Ameongeza kuwa: Siku ya Quds mwaka huu itaadhimishwa katika hali ambayo tunashuhudia uimara wa wanamapambano wa Palestina katika makabiliano makali sana na utawala wa Kizayuni. Ulimwengu mzima umeshuhudia jinsi utawala wa Kizayuni ulivyoua kikatili zaidi ya watu 50,000, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, na unavyoendelea kuharibu makumi ya vituo vya afya na kuweka mzingiro mkubwa dhidi ya Wapalestina wa Ghaza. Hata alipoingia madarakani rais mpya wa Marekani naye pia ameupa zawani utawala wa Kizayuni nayo ni zawadi ya kutumia silaha kali zaidi za kuua kwa umati wananchi wa Hhaza ili kuwalazimisha wahame kwenye eneo lao hilo. Lakini amesema: Wanachoshindwa kujua Wazayuni ni kwamba fikra za Hamas na Muqawama zimekita mizizi na kamwe hazitatoweka hata wakiendelea kufanya unyama wa kuchupa mipaka dhidi ya Wapalestina.
342/
Your Comment