27 Machi 2025 - 15:51
Source: Parstoday
Hamas yataka walimwengu wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono Palestina Siku ya Quds

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa mwito wa kuhamasishwa walimwengu kujitokeza kwa wingi katika siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ili kuonyesha mshikamano na Gaza na al-Quds wakati huu ambapo Israel, kwa uungaji mkono wa Marekani, inaendelea na vita vyake vya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina Gaza, mkabala wa kimya cha dunia.

Katika taarifa yake, Hamas imetoa mwito wa "Kuongezeka na kuendelea kwa aina zote za mikusanyiko na maandamano ya kuonyesha mshikamano (na Wapalestina) katika kila kituo, jiji na miji mikuu duniani kote."

Hamas imesema, "Tunatoa wito kwa umati wa watu wetu wa Palestina, mataifa ya Kiarabu na Kiislamu, pamoja na watu wote walio huru duniani kote, kukusanyika Ijumaa ijayo, na pia Jumamosi, na Jumapili kuzilinda Gaza, al-Quds, na al-Aqsa, kuunga mkono ustahimilivu wa watu wetu, kupinga jinai na mipango ya uvamizi dhidi ya ardhi yetu, watu na maeneo matakatifu, na kuilaani Marekani kwa uungaji mkono wake kwa ukatili huu (unaofanyika Gaza)."

Harakati hiyo ya Muqawama imesisitiza haja ya njia zote zinazowezekana kutumika kuvunja mzingiro wa Gaza, kukomesha mauaji na njaa huko Gaza. Imebanisha kuwa, juhudi na nguvu zote zinapaswa kuelekezwa kusaidia Gaza, kuponya makovu yake, na kuimarisha uthabiti wake." 

Hamas yataka walimwengu wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono Palestina Siku ya Quds

Aidha kundi hilo linalopigania ukombozi wa Palestina limetaka kuwepo mshikamano na al-Quds na al-Aqsa, likihimiza kuwepo mashinikizo mtawalia dhidi ya Israel na kufichuliwa jinai za utawala huo vamizi, ukiwemo uungaji mkono wa Marekani kwa utawala huo, hadi uchokozi na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina yatakapokomeshwa.

Wakati huo huo, Ziad Al-Nakhala, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina ametoa hotuba kwa mnasaba wa maandalizi ya Siku ya Kimataifa ya Quds akiwapongeza mashahidi wa Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa na kusema: "Malengo yetu ni ya hali ya juu na adhama yetu ni kubwa. Al-Nakhala ameeleza kuwa: Wazayuni wauaji na washirika wao hawawezi kuvunja irada yetu, na tunazidi kuwa na nguvu. Muqawama wetu unaweka historia isiyosahaulika leo hii.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha