Ripoti kutoka Ghaza zinaeleza kuwa, mbali na kumuua shahidi al-Qanoua, shambulio hilo lililolenga hema limejeruhi pia watoto kadhaa katika eneo hilo.Abdel-Latif Al-Qanoua ni kiongozi mwingine mwandamizi wa Hamas aliyeuliwa shahidi katika jinai ya karibuni zaidi iliyofanywa na jeshi la Israel tangu lilipoanzisha upya vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Ghaza.
Mapema wiki hii, jeshi la Kizayuni liliwaua viongozi wawili waandamizi wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Ismail Barhoum na Salah al-Bardaweel, katika mashambulizi ya kigaidi yaliyolenga hospitali na hema.
Kwa mujibu wa Hamas, kabla ya hapo utawala wa Kizayuni ulishawaua shahidi viongozi tisa waandamizi wa ofisi ya kisiasa ya harakati hiyo ya ukombozi wa Palestina.Viongozi hao ni Ismail Haniya, Yahya Sinwar, Saleh al-Aruri, Rawhi Mushtaha, Sameh al-Sarrah, Marwan Issa, Zakariyya Muammar, Jamila ash-Shanti na Jawad Abu Shammala.
Wakati huohuo, ripoti nyingine kutoka Ghaza zinaeleza kwamba familia nzima ya watu sita imeuawa shahidi wakati wanajeshi wa Kizayuni walipoliripua kwa bomu jengo la ghorofa la familia ya al-Gharbawi katika eneo la as-Saftawi katika Mji wa Ghaza.
Sambamba na hayo, katika muda wa saa chache zilizopita, Wapalestina wengine tisa wameuawa shahidi na makumi ya wengine wamejeruhiwa huku hospitali za Ghaza zikishindwa kufanya kazi kwa sababu ya kuelemewa na idadi kubwa ya majeruhi na ukosefu wa vifaa vya matibabu, unaotokana na hatua ya Israel ya kuzuia kikamilifu kuingizwa chochote katika eneo hilo kwa zaidi ya wiki tatu sasa.
Hayo yanajiri huku Wizara ya Afya ya Gaza ikitangaza kuwa, Wapalestina 50,183 wamethibitishwa kuuawa shahidi na wengine 113,828 kujeruhiwa katika vita vya kinyama na mauaji ya kimbari ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Ghaza. Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Serikali ya Gaza imesasisha idadi ya waliouawa shahidi na kusema wameshapindukia 61,700 kutokana na maelfu ya Wapalestina waliotoweka chini ya vifusi kukadiriwa kuwa wameshafariki dunia.../
342/
Your Comment