28 Machi 2025 - 17:36
Source: Parstoday
Jibu la Iran kwa barua ya Trump/ Araqchi: Mazungumzo chini ya mashinikizo hayana maana

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Iran amesisitiza kwamba mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani kuhusu mpango wa amani wa nyuklia wa nchi hiyo hayana maana maadamu sera ya "shinikizo la juu" na vitisho vya kijeshi bado vipo.

Sayyid Abbas Araqchi Waziri amesema kuwa jibu rasmi la Iran kwa barua ya Rais Donald Trump wa Marekani limetolewa ipasavyo kupitia Oman. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Jibu rasmi la Iran linajumuisha barua ambayo ndani yake Tehran imeeleza misimamo na maoni yake kuhusu  hali ya sasa; na barua ya Trump imefafanuliwa kikamilifu, na upande wa pili umejulishwa. 

Araqchi amesisitiza kuwa: Sera ya Iran ni kutofanya mazungumzo ya moja kwa moja chini ya mashinikizo ya kiwango cha juu na vitisho vya kijeshi lakini mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yanaweza kuendelea kama ilivyokuwa huko nyuma. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran jana usiku alizungumza kwa simu na David Lammy Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Uingereza na kuashiria kufanyika duru nne za mazungumzo kati ya jumbe zinaoiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi tatu za Ulaya. Alieleza kusikitishwa kwake na baadhi ya harakati na misimamo hasi ya nchi za Ulaya na Umoja wa Ulaya, ikiwemo kutekelezwa na kuendelezwa vikwazo vya aiina mbalimbali dhidi ya Iran kwa visingizio visiyo na msingi, na kuzitaka nchi hizo tatu za Ulaya zitazame upya misimamo yao kuhusiana na Jamhuri ya Kiislamu na masuala ya eneo la Magharibi mwa Asia.

Jibu la Iran kwa barua ya Trump/ Araqchi: Mazungumzo chini ya mashinikizo hayana maana

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza pia amempongeza waziri mwenzake wa Iran kwa kuwadia mwaka mpya wa 1404 Hijria shamsia na kusisitiza kuwa Uingereza na nchi nyingine za Ulaya zimedhamiria kutafuta suluhu ya kidplomasia la kadhia ya nyuklia ya Iran.  

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha