30 Machi 2025 - 17:27
Source: Parstoday
Mtaalamu: Badala ya kusimamia haki, ICC inatumikia madola yenye nguvu

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imepoteza uhalali wake kwa kutumikia maslahi ya kisiasa ya madola fulani. Hayo yameelezwa na Ali Hammoud, mtaalamu wa mahusiano ya kimataifa wa Kituo cha Mafunzo ya Kidiplomasia na Kimkakati (CEDS) chenye makao yake mjini Paris, Ufaransa.

ICC, yenye makao yake makuu The Hague imekabiliwa na ukosoaji katika miaka ya hivi karibuni kwa kushindwa kuwapandisha kizimbani watu kutoka mataifa yenye nguvu zaidi na badala yake kuwaandama wale wanaotoka mataifa ya Asia na Afrika.

Katika mahojiano na chaneli ya televisheni ya Russia Today Hammoud amesema, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai inatumia vipimo vya kindumakuwili na inatumikia madola yenye nguvu duniani badala ya kusimamia haki.

"Ili ICC irejeshe uhalali na itibari yake lazima ionyeshe kwamba hakuna yeyote aliye juu ya sheria, bila kujali utaifa wake na mahusiano yake ya kisiasa na wengine", ameeleza Hammoud.

Mnamo Novemba 2024, ICC ilitoa hati ya kukamatwa waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu kwa kuhusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa wakati wa vita katika Ukanda wa Ghaza.

Hata hivyo hadi sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya Netanyahu, huku utawala haramu wa Israel ukiendeleza mashambulizi ya kinyama na mauaji ya kimbari katika eneo hilo na kushadidisha mashambulizi hayo kuanzia mapema mwezi huu baada ya kuvunja mapatano ya usitishaji vita iliyofikia na harakati ya Hamas.

Licha ya shutuma za kuhusika na mauaji ya kimbari na uangamizaji wa kizazi cha Wapalestina, utawala wa Kizayuni unaendelea kuungwa mkono kwa hali na mali na madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha