Brigedia Jenerali Yahya Saree, msemaji wa jeshi la Yemen, ametangaza hayo leo Jumapili asubuhi na kusisitiza kuwa, vikosi vya jeshi la nchi hiyo vimefanya operesheni tatu kubwa za kijeshi za kuzitwanga meli za Marekani katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Jenerali Saree amebainisha kuwa, operesheni za kulipiza kisasi zilizofanywa dhidi ya manuwari na meli za kivita za Marekani kwenye Bahari ya Sham zimehusisha kikosi cha makombora, kitengo cha ndege zisizo na rubani cha jeshi la anga pamoja na kikosi cha wanamaji cha jeshi la Yemen. Operesheni hizo zimeendeshwa kwa kutumia makombora mengi ya kivita yaliyotengenezwa nchini Yemen pamoja na kundi la droni.
Afisa huyo wa ngazi za juu wa kijeshi wa Yemen amesisitiza kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo ya Kiarabu vitaendelea kukuza uwezo wake wa kiulinzi na vitakabiliana vilivyo na jinai zinazoongezeka kila kukicha za adui hasa Marekani. Amesisitiza kwamba majeshi ya Yemen hayatarudi nyuma katika kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Palestina hadi mashambulizi ya umwagaji damu yanayoendelea kuafanya na Israel dhidi ya Ghaza yatakapokoma, na mzingiro wa eneo la utakapoondolewa kabisa.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, hakuna suluhisho la kijeshi kwa mgogoro wa Yemen. Amepongeza ushujaa wa vikosi vya ulinzi vya Yemen katika safu zao zote, akisema vinatekeleza majukumu yao ya kidini, kibinadamu na maadili katika kulinda Yemen huru na kuunga mkono Wapalestina wanaodhulumiwa.
342/
Your Comment