Katika taarifa yake ya leo Jumapili, HAMAS imesema: "Katika siku ya Idul Fitr, tunapongeza na kujivunia uimara wa taifa letu kubwa na Muqawama wake wa kijasiri na tunamuomba Mwenyezi Mungu alete utulivu na ustahimilivu zaidi."
Taarifa hiyo ya Hamas aidha imesema: "Idul Fitr ya mwaka huu imekuja katika wakati ambapo wananchi wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza, Ukingo wa Magharibi na Baytul Muqaddas wako chini ya uvamizi, mzingiro, njaa, mauaji na jinai zinazofanywa kimataifa dhidi yao kwa uungaji mkono kamili wa Marekani kwa adui vamizi."
Hamas pia imepongeza Muqawama wa wananchi wa Palestina hasa huko Ghaza licha ya kwamba wako chini ya mzingiro na jinai za kutisha za Israel. Vilevile imepongeza uimara wa Wapalestina wa Ukingo wa Magharibi, Baytul Muqaddas na ndani ya maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni tangu mwaka 1948 katika kukabiliana na jinai, ubaguzi na akhabithi wa kila aina ya Israel.
Vilevile katika taarifa yake hiyo, Hamas imetoa mwito kwa Ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu kufanya juhudi zaidi na kuongeza uungaji mkono wao kwa watu wa Palestina hasa wa huko Ghaza na kuwajibika katika kuishinikiza Israel ikomeshe jinai zake, iache kuizingira Ghaza na kusaidia mapambao ya ukombozi wa haki ya Palestina hadi ushindi upatikane na uvamizi huo ukomeshwe.
342/
Your Comment