Hatua hiyo ya kijuba ya adui Mzayuni imekuja wakati Hamas ilikuwa imetangaza huko nyuma kwamba imekubali pendekezo la wapatanishi na kusisitiza kuwa silaha za Muqawama ni mstari mwekundu. Utawala wa Kizayuni unaoukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina unaendelea kuvuruga makubaliano ya kubadilishana mateka na unaendelea kufanya mauaji ya kutisha na ya kinyama dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Ghaza.
Vyombo vya habari vya Kizayuni vimetangaza kwamba Tel Aviv imekataa pendekezo la wapatanishi na imetaka kuachiliwa huru mateka kumi wa Israel badala ya watano katika pendekezo la Misri.
Ofisi ya waziri mkuu wa wa utawala wa Kizayuni wa Israel imetangaza kwamba, Benjamin Netanyahu, amefanya mlolongo wa vikao vya mashauriano kuitikia misimamo ya magenge yenye misimamo mikali ya Israel na mwisho amelikataa pendekezo hilo kwa baraka kamili za Marekani.
Khalil Hayyeh, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas alikuwa ameelezea matumaini yake kwamba baada ya Hamas kukubaliana na pendekezo la Misri na Qatar, utawala wa Kizayuni hautokwamisha juhudi za wapatanishi.
Amesisitiza kuwa, Netanyahu amesimamisha awamu ya pili ya mazungumzo ya kusitisha mapigano ili kulinda serikali yake na kuepusha kutimuliwa madarakani lakini HAMAS inaendelea kuheshimu ahadi zake.
Vile vile amesisitiza kuwa, Muqawama hautaacha hatima ya Wapalestina mikononi mwa wavamizi Wazayuni, bali utaendeleza mapambano hadi ukombozi kamili.
342/
Your Comment