Sheikh Naim Qassem amesema hayo na kubainisha kuwa, "Rouhullah Imam Khomeini alitangaza [Ijumaa ya mwisho ya kila Ramadhani] kuwa siku ya kimataifa ya kukabiliana na ukandamizaji na dhulma."
Ameendelea kufafanua kwa kusema, "Kwa mujibu wa Imam Khamenei, kadhia ya Palestina si mbinu ya kisiasa, bali ni suala la imani, moyo na imani," amesema na kuongeza, "Siku hii inaanzia Palestina hadi ulimwengu mzima, lakini sehemu yake kuu inabaki kuwa Palestina."
Kiongozi huyo wa Hizbullah pia amebainisha kuwa, tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hadi sasa, kipindi ambacho kimekuwa na uungaji mkono wa dhati wa Iran kwa kadhia ya Palestina na Jamhuri ya Kiislamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya kuendeleza uungaji mkono wa Wapalestina duniani kote, "mabadiliko mengi yametokea kwa ajili ya Muqawama" dhidi ya ukatili wa Israel.
Amehimiza Siku ya Quds iadhimishwe duniani kote kila mwaka kwa mujibu wa ushauri wa Imam Khomeini kama "wajibu wa kidini na kiitikadi unaovuka mipaka na siasa."
Ameongeza kuwa, "Siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ya mshikamano na [mji mtakatifu wa] al-Quds unaokaliwa kwa mabavu na watu wote wanaodhulumiwa duniani kote mbele ya madola ya kibeberu, wavamizi, wanaokula njama na madhalimu."
342/
Your Comment