30 Machi 2025 - 17:34
Source: Parstoday
HAMAS: Tumekuwa na mazungumzo ya mfululizo na wapatanishi kwa ajili ya kusitishwa vita Ghaza

Bassem Naim, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amethibitiha kuwa katika siku za karibuni, harakati hiyo ya ukombozi wa Palestina imekuwa na mazungumzo ya mfululizo na wapatanishi yanayolenga kutekelezwa tena usitishaji vita katika Ukanda wa Ghaza

Naim amesema: "tunatumai kuwa, mnamo siku chache zijazo tutashuhudia mafanikio ya kweli katika vita baada ya mazungumzo ya mafululizo na wapatanishi katika siku za hivi karibuni."Duru za karibu na Hamas zimevieleza vyombo vya habari kuwa mazungumzo yalianza Alkhamisi jioni kati ya harakati hiyo ya Muqawama na wapatanishi kutoka Misri na Qatar mjini Doha ili kufufua usitishaji vita na kuachiliwa mateka wa Israel ambao wangali wanashikiliwa huko Ghaza.

Kwa mujibu wa Basim Naim, pendekezo lililojadiliwa katika mazungumzo hayo ni kufikia makubaliano ya kusitisha vita, kufunguliwa vivuko, kuruhusu uingizaji misaada, na muhimu zaidi, kurudi kwenye mazungumzo ya kujadili awamu ya pili, ambayo itapasa ipelekee kusimamishwa vita kikamilifu na kuondoka vikosi vya utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.

Mnamo Machi 18, jeshi la utawala wa Kizayuni lilivunja makubaliano ya kusitisha vita kwa kuanza tena kuushambulia kwa makombora Ukanda wa Gaza na kisha kuanzisha oparesheni za uvamizi wa ardhini, miezi miwili tangu utawala ghasibu wa Israel na harakati ya Hamas zilipofikia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Mazungumzo kuhusu awamu ya pili ya makubaliano hayo yamekwama, kutokana na Israel kutaka urefushwe muda wa utekelezaji wa awamu ya kwanza ya usitishaji mapigano, huku Hamas ikitaka yafanyike mazungumzo ya utekelezaji wa awamu ya pili kama ilivyoagizwa katika makubaliano, hatua itakayopelekea kusitishwa vita kikamilifu.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Ghaza, watu wasiopungua 896 wameuawa shahidi katika Ukanda huo tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha tena mashambulizi yake.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha