30 Machi 2025 - 17:34
Source: Parstoday
Katika maadhimisho ya Siku ya Quds Indonesia na Malaysia; Mahathir miongoni mwa waandamanaji

Waislamu na watetezi wa haki duniani katika nchi za Indonesia na Malaysia wameshiriki kwa maelfu katika maandamano ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds yanayofanyika katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwenye pembe mbalimbali za dunia.

Maelfu ya wananchi wa Malaysia na Indonesia siku ya Ijumaa walimiminika mabarabarani kuunga mkono piganio tukufu la Palestina.

Nchini Indonesia katika mji mkuu Jakarta na miji mingine ya nchi hiyo, waandamanaji walipiga nara dhidi ya utawala wa Kizayuni na kuunga mkono haki za wananchi wa Palestina.

Maandamano katika mji mkuu wa Indonesia yaliishia mbele ya ubalozi wa Marekani ambapo wananchi wa taifa hilo la Kusini Mashariki mwa Asia walitaka kukomeshwa misaada ya silaha ya Washington kwa utawala ghasibu wa Kizayuni.Wananchi wa Indonesia wametoa wito pia wa kuchukuliwa hatua za haraka na jamii ya kimataifa na mashirika ya kimataifa ili kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ghaza.

Nchini Malaysia pia, maandamano ya Siku ya Quds yalifanyika jana karibu na Ubalozi wa Marekani mjini Kuala Lumpur.Wananchi wa Malaysia wamelaani hatua za serikali ya Marekani za kuunga mkono uvamizi, uchokozi na jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina.

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Mahathir Mohamad naye pia alishiriki kwenye maandamano ya nchini humo ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds.Jana (Ijumaa), Machi 28, 2025 (Farvidin 8, 1404 AH), ilisadifiana na Ramadhani ya 27, 1446 Hijria ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds.

Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani imepewa jina la Siku ya Kimataifa ya Quds kwa ubunifu wa Imam Khomeini (RA), mwasisi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ili Waislamu duniani kote waweze kudhihirisha chuki zao kwa siasa za kibaguzi za utawala wa Kizayuni.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha