31 Machi 2025 - 22:07
Source: Parstoday
Majeshi ya Iran yaahidi ‘Majibu Makali’ kwa tishio lolote

Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema iko tayari kutoa jibu kali na lenye nguvu dhidi ya tishio lolote, uchokozi, au uvamizi maadui.

Katika taarifa iliyotolewa katika kumbukumbu ya mwaka wa 46 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Kiislamu, jeshi la Iran lilisema siku ya Jumapili kuwa Iran imekuwa ikitetea misingi yake na taifa lake kwa nguvu kila mara, na imekuwa mjumbe wa amani na usalama wa kikanda na kimataifa.

Taarifa hiyo ilionya maadui wote waliokosea mahesabu yao kuwa tishio lolote, uchokozi, uchochezi wa vita au uvamizi wa ardhi ya Iran utajibiwa kwa nguvu  na kwa mtazamo wa kuhujumu.

Taarifa hiyo imesema Iran imekuwa ikifuata mkakati wa kudumu wa kujihami na kuunga mkono watu wanyonge duniani, hasa watu wanaodhulumiwa wa Palestina, kama mkakati “usio na mabadiliko na wa dhati kabisa.”

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Jamhuri ya Kiislamu imefikia kiwango cha juu cha uwezo wa kijeshi wa kujihami na endelevu, na haitasita kamwe kufuatilia malengo yake matakatifu mbele ya mashinikizo yoyote, vitisho, au matamshi yasiyo na maana kutoka kwa vyombo vya utawala wa kiimla duniani.

Kamandi ya  Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema: "Tangu miaka ya mwanzo ya kuanzishwa kwake, Iran ilikumbana na uadui mkubwa na njama mbalimbali, pamoja na hila mbaya zaidi kutoka kwa madola ya kiistikbari yanayoongozwa na Marekani."

Pia imesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu imegeuka kuwa mfumo madhubuti na thabiti kwa misingi ya nguvu ya kitaifa na mamlaka kamili, na vilevile kuwa nguvu yenye ushawishi mkubwa katika medani ya kimataifa na dunia nzima.

Zaidi ya asilimia 98.2 ya Wairani waliokuwa na haki ya kupiga kura walipiga kura ya ‘ndiyo’ katika kura ya maoni ya kihistoria ya mwaka 1979, ambapo walikubwa kuanzishwa kwa Jamhuri ya Kiislamu.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliundwa kwa mujibu wa kaulimbiu maarufu ya Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979 iliyosema: “Uhuru, Kujitegemea na Jamhuri ya Kiislamu” kwa ajili ya taifa hilo.

Tangu wakati huo, taifa la Iran huadhimisha kila mwaka tarehe 12 ya mwezi wa Farvardin (kwa kalenda ya Iran) kama Siku ya Jamhuri ya Kiislamu.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha