Hamas imeeleza katika taarifa: "kuuawa watoto wadogo katika siku ya Idi kwenye kambi za wakimbizi kunadhihirisha ukubwa wa Ufashisti wa utawala ghasibu na jinsi utawala huo usivyo na chembe ya maadili ya kiutu na kiakhlaqi".
Jana Jumapili, ambayo ilikuwa siku ya kwanza ya Idul-Fitri huko Palestina, utawala wa Kizayuni uliwaua shahidi Wapalestina 64 wakiwemo watoto 13.Hamas imeongeza kuwa: mashambulizi hayo ya kigaidi katika siku ya kwanza ya Idul-Fitri yamepelekea kuuawa shahidi makumi ya watu, ikiwa ni pamoja na idadi ya watoto waliovalia nguo za Idi".
Taarifa ya Hamas imesisitiza kuwa: mauaji ya watoto katika siku ya Idi wakiwa kwenye mahema yao yanadhihirisha ufashisti wa utawala wa Kizayuni na jinsi utawala huo usivyo na chembe ya maadili ya kiutu na kiakhlaqi.Hamas imeongezea kwa kusema: "kinachomhamasisha mhalifu wa kivita Netanyahu kuendeleza jinai zake na kukiuka sheria za kimataifa ni kutofuatiliwa, kushindwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua na kimya chake cha kuaibisha inachoonyesha".../
342/
Your Comment