31 Machi 2025 - 22:13
Source: Parstoday
Rais wa Iran atoa mkono wa Idi kwa viongozi na wananchi wa mataifa ya Kiislamu

Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia salamu za mkono wa Idi na kuwapongeza viongozi na wananchi wa mataifa ya Kiislamu kwa mnasaba wa kuadhimisha na kushereheka Idul-Fitri, siku ya sherehe na furaha kubwa kwa Waislamu.

Katika ujumbe na salamu zake hizo kwa viongozi wa nchi za Kiislamu, Rais Pezeshkian amesema: Idul-Fitri ni dhihirisho la umoja na kuimarishwa mafungamano ya kidini na kijamii kati ya Waislamu na wakati wa kupatikana matunda ya dua zilizoombwa kwa ikhlasi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema anatumai kwamba, kheri na baraka za Sikukuu hii iliyojaa rehema na baraka, zitazidisha mshikamano baina ya mataifa ya Kiislamu, kupatikana amani na utulivu kati ya nchi za Kiislamu na kustawishwa zaidi uhusiano baina yao katika nyuga zote.Siku ya mwanzo ya mwezi wa Mfunguo Mosi, Shawwal ni siku ya Idul-Fitri, ya Waislamu kusherehekea kurejea kwenye hali ya asili, ya fitra na maumbile.

Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, Waislamu wenye Saumu huzisafisha nafsi na roho zao na uchafu wa nje na wa batini kwa kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuomba maghufira kwa madhambi yao, na hivyo kurejea kwenye asili na maumbile yao halisi.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha