31 Machi 2025 - 22:14
Source: Parstoday
Kiongozi wa Mapinduzi: Utawala fisadi wa Israel ni ‘kikosi cha niaba tu’ katika eneo, ni lazima ung'olewe

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, kikosi pekee cha niaba katika eneo hili ni utawala wa Kizayuni ambao unavamia nchi nyingine kwa niaba ya madola ya kikoloni ya dunia na ni "lazima ung'olewe."

Ayatullah Khamenei ameeleza hayo katika khutba za baada ya Sala ya Idul-Fitri iliyosaliwa leo asubuhi katika Uwanja Mkuu wa Mosalla wa Imam Khomeini mjini Tehran.

Sikukuu ya Idul-Fitri inaadhimishwa baada ya kumalizika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Wamagharibi wanawatuhumu vijana wenye ghera wa mataifa ya eneo hili kuwa ni wapiganaji wa niaba. Napenda nieleze kwamba, kuna kikosi kimoja tu cha niaba katika eneo hili ambacho ni utawala fisadi wa [Israel]" .

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa Israel inafanya mauaji ya kimbari na ikipatiwa fursa itavamia maeneo ya nchi nyingine kama ilivyoivamia Syria ikiwa ni kikosi cha niaba cha wakoloni.

Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwa kusema: "genge hili la wahalifu lazima ling'olewe katika Palestina na litang'olewa tu. Lazima kila mmoja afanye juhudi za kuufuta utawala huu muovu katika eneo".

Katika khutba hizo, Ayatullah Khamenei ameashiria pia vitisho inavyotoa Marekani dhidi ya Iran, na akaonya kwa kusema, hapana shaka yoyote, kitendo chochote kiovu kitakabiliwa na "kipigo kikali na cha kusagasaga".

"Ikiwa maadui wanafikiria kuchochea uasi wowote ndani ya nchi, taifa la Iran litawajibu," ameeleza Kiongozi wa Mapinduzi wa Kiislamu.Ayatullah Khamenei ameeleza kwa masikitiko pia kwamba matukio ya "umwagaji damu" huko Ghaza, Lebanon, na Yemen yameyafanya maisha ya watu kuwa machungu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha