"Esmail Baqaei," Msemaji wa Wizara ya mashauri ya Kigeni ya Iran ameandika ujumbe katika mtandao wa kijamii wa X akisema, Marekani lazima ikubali kwamba hatua yoyote dhidi ya Iran itakuwa na athari na matokeo yake na kuongeza kuwa: "Tishio la wazi na kiongozi wa nchi la kuishambulia Iran kwa mabomu ni ukiukaji wa wazi wa kiini cha amani na usalama wa kimataifa." Tishio kama hilo ni ukiukaji mkubwa wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa na ukiukaji wa mfumo wa ulinzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki. Utumiaji mabavu huzalisha utumiaji mabavu, na amani huleta amani. Marekani inaweza kuchaguzi (kati ya hayo mawili), lakini pamoja na matokeo yake", amesema Esmail Baqaei.
Ni baada ya Donald Trump kusema katika mahojiano ya simu na NBC News Jumapili, Aprili 1, kwamba "Iwapo Iran haitafanya mapatano na Marekani, itapigwa bomu katika hujuma ambayo haujawahi kushuhudiwa mfano wake."
342/
Your Comment