4 Aprili 2025 - 23:15
Source: Parstoday
Iran yalaani mashambulizi la Israel dhidi ya miundombinu ya raia na ulinzi ya Syria

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amelaani vikali hujuma ya kijeshi ya anga na ardhini ya utawala wa wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Syria na uharibifu wa vituo vya utafiti vya kiraia na kisayansi, pamoja na mlolongo wa miundombinu ya ulinzi ya nchi hiyo katika majimbo ya Damascus, Hama, Homs na Daraa.

Akigusia mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala wa Kizayuni na kulengwa maeneo muhimu zaidi ya ulinzi ya Syria na miundombinu ya kijeshi na ya kiraia sambamba na kukaliwa kwa mabavu maeneo muhimu ya kimkakati ya nchi hiyo ya Kiarabu kunakofanywa na utawala wa Kizayuni tangu kuanguka serikali ya zamani, Ismail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, kuna wajibu kwa pande zote kuulazimisha utawala wa Kizayuni kukomesha jinai zake hizo.

Amekumbusha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitahadharisha miezi kadhaa iliyopita katika mashauriano na nchi za eneo hili kuhusu Israel kutumia vibaya mazingira ya hivi sasa Syria na kupanua uvamizi na uchochezi wake dhidi ya nchi hiyo na nchi nyingine za eneo hili.

Baghaei amesisitiza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama ilivyokuwa hapo awali inatilia mkazo ulazima wa kuhifadhiwa na kulindwa umoja wa  ardhi, heshima na mamlaka ya kitaifa ya Syria kama taifa lenye mzizi wa kina na linalopigania utu katika eneo muhimu la Asia Magharibi. Pia ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa, hususan nchi za eneo hili kuimarisha Ushirikiano wa Kiislamu na kuuadhibu utawala wa Kizayuni kwa jinai zake ili uheshimu sheria na ukome kufanya mauaji ya kimbari katika ardhi za Palestina unazozikaliwa kwa mabavu.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha