Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) limetoa taarifa hiyo kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuuawa shahidi makamanda shupavu wa Kambi ya Muqawama na Mlinzi wa Haram Tukufu, Meja Jenerali Mohammad Reza Zahedi na Brigedia Jenerali Mohammad Hadi Haji Rahimi na maafisa wengine waliokuwa wameandamana nao, wakati utawala wa Kizayuni uliposhambulia kijinai jengo la ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Damascus Syria.
Katika taarifa yake hiyo ya jana Alkhamisi, Jeshi la SEPAHH limesema kuwa, kuuawa shahidi kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH huko Syria na Lebanon, Brigedia Jenerali Mohammad Reza Zahedi, na naibu wake, Mohammad Hadi Haji Rahimi, kwenye shambulio la Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, Damascus, tarehe 1 Aprili 2024 ni miongoni mwa vitendo vya fitna vya Wazayuni na viongozi wa Marekani katika eneo hili, lakini fitna hiyo haitaweza kusimamisha kasi kubwa na ya haraka ya kudidimia na kuporomoka utawala ghasibu wa Israel.
"Kwa msaada na taufiki ya Mwenyezi Mungu, Muqawama; hasa wa wapiganaji shupavu na majasiri wa Palestina, ambao sasa wanapata uungwaji mkono mkubwa na mshikamano wa mataifa kote ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na Ulaya na Marekani, hatimaye utakomesha maisha ya fedheha na machafu ya wavamizi wa Palestina," imeongeza taarifa hiyo.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH pia limesisitiza kuwa, kukombolewa Msikiti wa al-Aqsa ambao ni Qibla cha Kwanza cha Waislamu wa duniani kote, kutageuka kuwa kichwa kikuu cha habari za kimataifa kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu.
342/
Your Comment