6 Aprili 2025 - 23:59
Source: Parstoday
Maandamano ya malaki ya watu dhidi ya Trump na Musk kote Marekani

Jumamosi, maelfu Wamarekani walishiriki katika maandamano katika majimbo yote 50 ya Marekani, wakimpinga Rais Donald Trump na bilionea Elon Musk.

Takriban watu 500,000 walikusanyika katika maeneo zaidi ya 1,200, ikiwa ni pamoja na miji mikubwa kama New York na Washington, D.C wakipinga sera za Donald Trump.

Maandamano hayo yalilenga kupinga utawala wa Trump na ushawishi wa Idara ya Ufanisi wa Serikali (DOGE) katika maamuzi ya serikali.

Mwandamanaji James Utt, mwenye umri wa miaka 60 kutoka Los Angeles, ameeleza kwamba hadi sasa hajaamini kwamba Trump amechaguliwa tena na kuungana na mabilionea, na kuongeza kuwa mtawala huyo ameathiri vibaya uchumi wa Marekani.

Naye Kristen Messina kutoka Santa Monica amesisitiza umuhimu wa kulinda demokrasia, wakati wengine kama mtaalamu wa sayansi ya biomedikali aliyestaafu, Terry Klein wakieleza wasiwasi wao kuhusiana na sera za Trump za uhamiaji, elimu, na ushuru.

Wandamanaji walibeba mabango yaliyosema “achana na demokrasia yetu” na “simuamini Elon Musk,”

Barani Ulaya, maandamano dhidi ya Trump yalifanyika pia katika miji kama Berlin na London, yakionyesha kutoridhika kwa watu kuhusu sera za Trump.

Maandamano ya malaki ya watu dhidi ya Trump na Musk kote Marekani

Maandamano haya, ambayo yalikuwa makubwa zaidi tangu Trump arejee madarakani Januari mwaka huu, yamechochewa na wasiwasi kuhusu sera za uhamiaji, kurudisha nyuma sheria za mazingira na ushawishi wa kisiasa wa bilionea Elon Musk katika sera na maamuzi ya serikali ya Washington.

Wakati Trump alipokuwa akicheza gofu Florida, waandamanaji walikusanyika karibu na makazi yake ya Mar-a-Lago wakitangaza hasira zao kutokana na utawala wake mbovu.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha