10 Aprili 2025 - 19:52
Source: Parstoday
Maariv : Hamas bado inadhibiti Ukanda wa Gaza

Vyombo vya habari vya Kizayuni vimekiri kuwa, zaidi ya mwaka mmoja na nusu tangu kuanza vita na mshambulizi ya kijeshi dhidi ya Ukanda wa Gaza, harakati ya Hamas bado inadhibiti eneo hilo na utawala wa Kizayuni umeshindwa kufikia malengo yake.

Gazeti la Kizayuni la Maariv limemnukuu mchambuzi wake, Avi Ashkenazi akisema kuwa, mwaka mmoja na nusu baada ya kuanza hujuma za kijeshi, harakati ya Hamas ya Palestina bado ina udhibiti kamili wa Ukanda wa Gaza. Licha ya jeshi la Israel kufanya uharibifu mkubwa na kuyakalia kwa kamavu baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Gaza lakini viongozi wa Israel wamekiri kuwa wameshindwa kutimiza malengo yao ikiwa ni pamoja na kuwarejesha nyumbani mateka wao 59 wanaoshikiliwa na Hamas. 

Ashkenazi amesema kuwa jeshi la Israel limefanikiwa tu kuharibu karibu asilimia 25 ya njia za chini ya ardhi za harakati ya Hamas mbazo zina nafasi muhimu na kuu katika stratejia ya ulinzi na mashambulizi ya harakarti ya Hamas. 

Katika upande mwingine, gazeti la Kizayuni la Haaretz limenukuu tathmini iliyofanywa na duru za  usalama za Israel na kuripoti kuwa Harakati ya Mapambano ya Kislamu ya Palestina, Hamas, imerekebisha mbinu zake za kivita na hivi sasa inajizuia kutuma wapiganaji kwenye mahandaki hayo. Kwa sababu baadhi ya njia hizo za chini ya ardhi zinadhibitiwa na jeshi la Israel. 

Maariv : Hamas bado inadhibiti Ukanda wa Gaza

Gazeti hilo limeongeza kuwa: Hamas sasa imejielekeza katika kutengeneza na kuunda mabomu na mada za milipuko. 

Gazeti la Kizayuni la Haaretz limeendelea kueleza kuwa, Hamas imefanikiwa kuajiri na kutoa mafunzo kwa vijana na wapiganaji wapya takriban 40,000; Hatua inayodhihirisha kukarabatiwa nguvu za kijeshi za harakati hiyo licha ya mashinikizo makali ya kijeshi kutoka kwa utawala wa Kizayuni na washirika wake.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha