10 Aprili 2025 - 19:55
Source: Parstoday
Viongozi wa Amerika ya Latini watoa wito kupinga ushuru wa Trump

Viongozi wa nchi za Amerika ya Latini wametaka kuweko umoja na mshikamano wa kukabiliana na ushuru wa Rais Donald Trump wa Marekani na kuyumba uchumi kunakosababishwa na hatua hizo za Trump.

Ombi hili la nchi za Amerika ya Latini limetolewa wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Amerika Kusini na Caribbean (CELAC) yenye wanachama 33 katika mji mkuu wa Honduras, mkutano ambao ulihudhuriwa pia na China.

Viongozi 11 kutoka nchi za Amerika ya Latini na Caribbean wameishiriki katika mazungumzo hayo akiwemo Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, na Rais wa Mexico, Claudia Sheinbaum, nchi mbili zenye uchumi mkubwa zaidi  za Amerika ya Kusini, pamoja na Rais wa Colombia, Gustavo Petro, na Rais wa Honduras, Xiomara Castro. 

Rais Xiomaro Castro wa Honduras amesema: Hatuwezi kuendelea na njia yetu bila umoja pale Ulimwengu unapojipanga upya. 

Rais wa Honduras ameongeza kuwa: Marekani  imechora upya ramani yake ya kiuchumi bila kuzingatia watu walio katika mazingira magumu.

Rais wa Mexico, Claudia Sheinbaum pia mesema: Uchumi wa eneo la Amerika ya Latini unapasa kubadilisha masoko yao na kuzingatia zaidi "muungano na kusaidiana."

Kufuatia kusitishwa kwa siku 90 kwa ushuru wa  bidhaa zinazoingia Marekani kutoka nchi mbalimbali duniani, isipokuwa China ambayo imeongeza ushuru kwa bidhaa kutoka Marekani, Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa: Marekani inaweza kufikia mapatano na China na kwamba China inataka kufikia makubaliano lakini haijui itafanyaje. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha