Kile kinachojulikana kama "50501", ikimaanisha "maandamano 50, majimbo 50, na kundi 1 la vuguvugu", maandamano hayo yalikusudiwa kwendana na kumbukumbu ya miaka 250 ya kuanza kwa Vita vya Mapinduzi vya Marekani.
Nje ya Ikulu ya White House na Tesla dealerships na katika vituo vya miji mingi, waandamanaji walitoa malalamiko mbalimbali. Wengi walitoa wito wa kurejeshwa kwa Kilmar Ábrego García, ambaye alifukuzwa kimakosa hadi El Salvador.
Maandamano ya kisiasa yanazidi kuwa ya kawaida nchini Marekani ambayo yamekuwa yakivutia makumi kwa maelfu katika miji nchini kote.
Umaarufu wa Trump unaonekana kudorora, haswa linapokuja suala la uchumi. Alipoingia madarakani Januari, kiwango chake cha kukubalika na watu kilikuwa 47%, kulingana na Gallup lakini katika kura ya hivi majuzi ya Reuters/Ipsos ilionyesha kuwa umaarufu wake umepungua hadi 43%.
342/
Your Comment