25 Aprili 2025 - 22:48
Source: Parstoday
Israel katika ghadhabu baada ya ICC kukataa kusitisha hati za kukamatwa Netanyahu na Gallant

Uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wa kukataa ombi la Israel la kusitisha utekelezaji wa hati za kukamatwa Waziri Mkuu wa utawala huo, Benjamin Netanyahu na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Yoav Gallant umeikasirisha mno serikali ya Tel Aviv.

Netanyahu na Gallant wanasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa tuhuma za kufanya mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na jinai dhidi ya binadamu katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.

Akizungumzia uamuzi huo wa ICC, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Gideon Sa'ar amedai: "Tumesema tangu awali kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya The Hague haina na haijawahi kuwa na mamlaka ya kutoa hati za kukamatwa waziri mkuu wa Israel na waziri zamani wa ulinzi."

Mapema jana, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ilitangaza kwamba imekataa ombi la Israel la kusimamisha utekelezaji wa waranti wa kukamatwa Netanyahu na Gallant, ambao wanasakwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Israel katika ghadhabu baada ya ICC kukataa kusitisha hati za kukamatwa Netanyahu na Gallant

Inafaa kukumbuka kuwa Israel ilikuwa imewasilisha ombi la kusitishwa utekelezaji wa hati za kukamatwa Netanyahu na Gallant, kwa madai kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kushughulikia kesi hiyo. Hata hivyo, chumba cha rufaa cha mahakama ya ICC kimesema ombi hilo "halina maana kwa sababu ya ukosefu wa msingi wa kisheria wa kuwasilishwa kwake."

Israel, ikisaidiwa na Marekani, imekuwa ikifanya mauaji ya kimbari huko Gaza tangu Oktoba 7, 2023, na hadi sasa imeua shahidi na kujeruhi karibu Wapalestina laki mbili, wengi wao wakiwa watoto na wanawake, na zaidi ya wengine 11,000 hawajulikani walipo.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha