Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Hawzat Imam Ali (a.s), iliyopo chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanga, Tanzania
Kitengo cha uhamasishaji wa Michango ya uwezeshaji wa masira ya Imam Husein (a.s) - Jumapili ya Leo, sawa na Tarehe 20 /04/ 2024 kimekutana na Waumini wa Bilal Muslim Boza na Bilal Muslim Mjimema.
Lengo la ziara hii, kuhamasishana na kuelezea umuhimu wa kutoa Sadaka hasa katika kuichangia Masira ya Imam Husen (a.s)
Katika ziara hii, Samahat Sheikh Swalehe AbduRahmani amewaeleza waumini fadhila za kutoa Sadaka na ubora wake.
Kitengo cha uhamasishaji kitaendelea na ziara hizi mpaka ndani ya Mwezi wa Muharram Insha'Allah.
Your Comment