21 Aprili 2025 - 23:01
Source: Parstoday
Mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Muqawama: Kuitetea Ghaza ni jukumu la Waislamu wote

Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Muqawama amesema, kuitetea na kuiunga mkono Ghaza ni jukumu la watu wote, na akatoa wito kwa mataifa ya Kiislamu na wanazuoni wa Kiislamu kuwasaidia ndugu zao wanaodhulumiwa huko Palestina na katika Ukanda wa Ghaza, wakati huu ambapo utawala wa Kizayuni wa Israel unaendeleza jinai zake dhidi yao.

Sheikh Maher Hammoud, amesema: "mauaji ya kimbari ya hivi sasa katika Ukanda wa Ghaza ni suala zito na kubwa ambalo halijawahi kushuhudiwa mfano wake katika historia. Kwa hiyo, tunayatolea wito mataifa ya Kiislamu duniani kufanya maandamano, kuonyesha mshikamano, na kutangaza misimamo yao katika kuwaunga mkono ndugu zao huko Ghaza".

Sheikh Hammoud aidha amewataka makhatibu, wasomi na wanafikra watekeleze jukumu lao la kuwasaidia watu wa Ghaza, na kutoa mwito wa kuungwa mkono kusimama nao bega kwa bega katika mateso yao, na kuwataka watawala wa nchi za Kiislamu pia watimize wajibu wao kuhusiana na suala hilo.

Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Muqawama amesema: "mzingiro huu, njaa, na mauaji ya makusudi na ya kuendelea dhidi ya watu wa Ghaza ni suala kubwa na muhimu ambalo umma unapaswa kusimama dhidi yake, na hakuna udhuru wowote utakaotolewa na mtu yeyote utakaokubalika, na kuna ulazima wa kutumia kila wenzo kwa ajili ya kuwatetea na kuwaunga mkono watu wa Ghaza"

Sheikh Hamoud amesifu pia operesheni za kishujaa zinazotekelezwa na Muqawama katika kukabiliana na hujuma za kinyama za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza na akawapongeza Mujahidina wa Palestina ambao wangali wana uwezo wa kuihami nchi yao licha ya hali mbaya na mazingira yote magumu yaliyoko katika Ukanda wa Ghaza.

Wizara ya Afya ya Ghaza imetangaza kuwa idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi kutokana na vita vya kinyama na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni kwa mwezi wa 18 sasa imefikia 51,201 na wengine 116,869 wamejeruhiwa.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha