Shirika la Hilali Nyekundu limepuuzilia mbali ripoti hiyo likisema ni batili na isiyokubalika, na kusisitiza kuwa imejaa uwongo.Imeongeza kuwa ripoti hiyo inalenga kuhalalisha mauaji na kutupia lawama za makosa kwenye kamandi ya operesheni huku ikipuuza ukweli halisi.
Jeshi la utawala wa Kizayuni lilidai jana Jumapili kwamba kulikuwa na "mapungufu kadhaa ya kitaaluma" katika mauaji ya watoaji huduma za dharura huko Ghaza, likisema kamanda wa jeshi aliyehusika ataachishwa kazi.Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina limeukataa uchunguzi huo uliofanywa na jeshi la Kizayuni na kusisitiza kuwa ripoti liliyotoa "imejaa uwongo".
"Ripoti imejaa uwongo. Ni batili na haikubaliki, kwa sababu inahalalisha mauaji na kuhamisha jukumu kwa makosa ya binafsi kwenye medani ya kamandi wakati ukweli halisi uko tofauti kabisa," ameeleza Nebal Farsakh, msemaji wa Hilali Nyekundu ya Palestina.
Mnamo Machi 23, wahudumu 15 Wapalestina wa sekta ya tiba na waokoaji waliuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la utawala wa Kizayuni karibu na Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza.Kupigwa risasi kikatili wafanyakazi hao ambao ni wahudumu wa afya na waokoaji kutoka Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Palestina, wa Ulinzi wa Raia wa Ghaza na mfanyakazi mmoja wa Umoja wa Mataifa kuliibua hasira kali kimataifa na miito ya kuchunguzwa uhalifu huo wa kivita.
Miili yao iligunduliwa wiki moja baadaye na maafisa wa Umoja wa Mataifa na wa Hilali Nyekundu katika kaburi lisilo na kina.../
342/
Your Comment