Mashambulizi ya anga ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza yamewaua Wapalestina wengine na hivyo kufanya idadi ya vifo kutokana na vita vya kinyama vya Israel vilivyoanza Oktoba 2023 kufikia 51,240.
Hayo ni kwa mujibu wa taaarifa ya Wizara ya Afya ya Palestina, ambayo imeongeza kuwa makumi ya watu wengine waliojeruhiwa walihamishiwa hospitalini, na kufanya jumla ya majeruhi kufikia 116,931 kutokana na mashambulizi ya Israel.
Taarifa hiyo imesema: “Waathirika wengi bado wamekwama chini ya vifusi na barabarani kwani waokoaji hawawezi kuwafikia."
Jeshi katili la utawala haramu wa Israel lilianza tena mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza mnamo Machi 18 na tangu wakati huo limewaua watu 1,630 na kuwajeruhi zaidi ya 4,300 licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano na kubadilishana wafungwa yaliyofikiwa Januari.
Mwezi Novemba uliopita, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wake wa zamani wa vita Yoav Gallant kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu huko Gaza.
Israel pia inakabiliwa na kesi ya mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutokana na vita vyake dhidi ya eneo hilo.
342/
Your Comment