Kwa mujibu wa Mtandao wa Al-Mayadeen, uhalifu ambao haujawahi kushuhudiwa unaofanywa na makundi yenye silaha katika maeneo ya mwambao wa Syria, ambao kama huo haujawahi kuonekana katika historia, unafanyika hivi sasa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, operesheni za mauaji ya halaiki zinafanyika katika vijiji vyote, na walioshuhudia wanatoa wito wa himaya ya kimataifa na kuundwa kwa kamati ya kimataifa ya kutafuta ukweli ili kufuatilia operesheni hizi katika maeneo ya pwani ya Syria.
Mashuhuda pia wanasema: Wauaji wanarekodi uhalifu wao katika maeneo ya pwani na kuchapisha na kujigamba juu yake. Jamii ya kimataifa lazima ituunge mkono, tulilipa gharama kubwa katika pwani ya Syria na bado tunalipa gharama bila kujua sababu.
Duru za ndani zimeripoti kuwa makundi ya wabeba silaha nchini Syria yanatelekeza maiti kwenye milima na mabonde ili kuficha uhalifu wao.
Baadhi ya vyombo vya habari pia viliripoti kuwa, makundi yenye mafungamano na Julani yaliwalazimisha wakaazi wa mji wa Barabsho huko Aleppo kukabidhi miili ya jamaa zao ili kuficha uhalifu wao na kuepuka kuandika mauaji hayo.
342/
Your Comment