Dmitry Bulatov Mkuu wa Muungano wa Taifa wa Russia wa Wauzaji Nje Bidhaa za Chakula amesema katika mahojiano na televisheni ya BRICS kuwa: Pendekezo la kuanzisha "Kituo cha Diplomasia ya Chakula" limetolewa ndani ya mfumo wa Kamati ya Kitaifa ya Utafiti ya BRICS ili kuratibu utekelezaji wa maamuzi yanayohusiana na kupanua ubadilishanaji wa bidhaa za chakula kati ya wanachama wa kundi hilo.
Bulatov amesema: Kituo cha Russia cha Diplomasia ya Chakula kinaweza kuwa na nafasi chanya katika kuhakikisha biashara ya kimataifa inakuwa endelevu.
"Upo ulazima kwa wataalamu wa nchi za BRIBS kutayarisha hati ya kimataifa ya maadili katika masoko ya chakula ili kutumika kama mfumo wa pamoja kwa nchi zinazofanya biashara ya kimataifa ya chakula," amesema Dmitry Bulatov Mkuu wa Muungano wa Taifa wa Russia wa Wauzaji Nje Bidhaa za Chakula.
Bulatov pia amesisitiza kuhusu nafasi kuu ya Russia katika kudhamini usalama wa chakula duniani na kusema nchi hiyo ni ya kwanza duniani katika mauzo ya ngano, na ni miongoni mwa nchi wasambazaji wakubwa wa nafaka duniani.
342/
Your Comment