Ismail Baqaei amesema, kuendelea mzingiro wa Ukanda wa Gaza na kuzuiwa misaada ya kibinadamu sambamba na kushadidisha mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya kambi na mahema ya wakimbizi ni mfano halisi wa jinai ya kivita na jinai dhidi ya ubinadamu na ametaka hatua madhubuti za kimataifa zichukuliwe ili kuwaadhibu viongozi wa utawala huo ghasibu kutokana na kutenda jinai za kivita na mauaji ya kimbari.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelikosoa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kutochukua hatua za kukabiliana na jinai hizo na kuzitaja Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zinazoendelea kutoa misaada ya silaha kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni washirika wa utawala huo katika jinai unazofanya.Ghaza
Baqaei pia amelaani vikali mashambulizi yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya mamlaka na ardhi ya Lebanon kupitia ukiukaji wa mara kwa mara wa makubaliano ya usitishaji vita, mashambulizi ya anga na ndege zisizo na rubani katika maeneo mbalimbali ya Lebanon, na mauaji ya wanaharakati wa kisiasa na kijamii nchini humo, na kusisitiza wajibu wa Umoja wa Mataifa na wasimamizi wa makubaliano hayo wa kusimamisha jinai hizo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "Kutoadhibiwa utawala wa Kizayuni wa Israel na kuendelea kuuawa watu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kukaliwa kwa mabavu baadhi ya maeneo ya Lebanon na Syria, kunatishia pakubwa amani na usalama katika eneo la Magharibi mwa Asia, na nchi za eneo hilo zinapaswa kuchukua hatua za dhati ili kuzuia hali ya ukosefu wa usalama na kukabiliana na sera za kupenda kujitanua za utawala huo ghasibu."
342/
Your Comment