Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha Ireland kilichopo Clonskeagh, Dublin, kilifungwa kufuatia tukio lililotokea mwishoni mwa wiki.
Tangazo lililowekwa kwenye lango la kituo kilisema kwamba kufuatia “tukio lenye kusikitisha sana” Jumamosi iliyopita, “hatuna budi ila kufunga kwa muda Msikiti na Kituo.”
Tangazo hilo lilielezea tukio la Jumamosi kama “shambulio lisilokuwa na mfano kwenye Msikiti wetu, Kituo na wajumbe wa Bodi.”
Hakukuwa na maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusiana na sababu ya kufungwa, lakini video zilizochukuliwa kutoka ndani na nje ya kituo mwishoni mwa wiki, na zilizotazamwa na gazeti la The Journal, zinaonyesha vurugu na kutoelewana kunakotokea.
Katika video hizo, wanaume wanaonekana wakipaza sauti na kushinikiza wakiwa wamesimama mbele ya wenzao. Polisi (Gardaí) pia walikuwepo ndani na nje ya kituo, na katika video moja wanaonekana wakimtoa mtu katika chumba baada ya kuzima mzozo.
Shaykh Dkt. Umar Al-Qadri, mwenyekiti wa Baraza la Waislamu wa Ireland, aliambia The Journal kwamba tukio hilo lilitokana na mzozo wa ndani.
Tangazo hilo lilisema Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha Ireland (ICCI) kitafungwa mpaka uchunguzi kamili wa matukio ya Jumamosi ukamilike na mipangilio ya usalama itekelezwe.
Tangazo kutoka kwa uongozi wa ICCI pia lilisema kwamba uamuzi wa kufunga msikiti ulikuwa umefanywa “kwa msisitizo mkubwa wa usalama wa jamii yetu, hasa watoto wa Shule ya Kitaifa ya Kiislamu.”
“Hii ni hali ya huzuni sana katika historia ya Msikiti wetu na Kituo,” ilisema taarifa hiyo.
Wakati sababu ya kufungwa ikibaki kutokuwa wazi, ombi la mtandaoni lilianzishwa Jumanne likiwa na anuani ya “Okoa msikiti wetu ICCI Usifungwe.” Ombi hilo tayari limetiwa saini na zaidi ya watu 1,800.
Polisi waliambia The Journal mapema kwamba hawakuhusika katika jambo lolote kwenye kituo hicho.
342/
Your Comment