Esmail Baqaei alieleza hayo jana Jumatatu mjini Tehran katika mkutano wa kila wiki na waandishi wa habari, akizungumzia ziara ya ujumbe wa kiufundi wa IAEA nchini Iran.
"Safari hii ya ujumbe wa kiufundi wa wakala wa IAEA ni mwendelezo wa mazungumzo ya wiki jana kati ya maafisa wa Iran na IAEA," amesema Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran.
Baqaei pia amedokeza kuhusu mazungumzo kati ya Iran na Marekani kwamba duru ijayo ya mazungumzo hayo yasiyo ya moja kwa moja kati ya pande mbili imepangwa kufanyika Jumamosi ijayo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na nchi mwenyeji, Oman.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza pia msimamo wa Iran mkabala wa miradi yake ya nyuklia inayofanyika kwa malengo ya kiraia na vikwazo haramu dhidi ya nchi hiyo. "Suala la kurutubisha urani na kuondolewa vikwazo kikamilifu ni mistari myekundu katika mazungumzo na Marekani," amesema Baqaei.
Alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu ziara za karibuni za Waziri wa Mambo ya Nje huko Beijing na Moscow, amesema: Masuala ya uhusiano wa pande mbili na mauaji ya kimbari ya Israe dhidi ya watu wa Gaza zilikuwa ajenda kuu za mashauriano wakati wa ziara ya Sayyid Abbas Araqchi huko China na Russia.
342/
Your Comment